Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Bw. Deo Mwanyika, Makamu wa Rais
wa Kampuni ya Barrick Tanzania baada ya kuibuka mchangiaji mkubwa kwa
kutoa dola za Kimarekani laki 5 kwa ajili ya kuchangia taasisi ya Mkapa
Hiv/Aids Foundation Jumanne Juni 5, 2012 usiku katika hoteli ya
Kilimanjaro jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya
Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu
Mzee Benjamin William Mkapa aliyeandaa hafla hiyo iliyoweza kukusanya
shilingi bilioni 3.2 na kuvuka malengo ya harambee hiyo kwa asilimia
sita
Rais
Jakaya Kikwete, akimkabidhi picha ya kuchora Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya UNDI Consulting Group Limited, Bw Philip Makoka aliyoinunua
kwa shilingi milioni 20 wakati wa Harambee ya kuchangia fedha programu
ya Mkapa Fellows inayoendeshwa naTaasisi ya Mkapa HIV/AIDS iliyofanyika
Dar es Salaam kwenye hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar
es salaam. Kulia ni mchoraji wa picha hiyo, Bwana Muzu
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya
Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na Rais Mstaafu wa Awamu ya
Tatu Mzee Benjamin William Mkapa baada ya kuwa mgeni rasmi katika
harambee ya kuchangia Taasisi ya Mkapa HIV/AIDS foundation na kusaidia
kukusanya shilingi bilioni 3.2 nauvuka malengo ya harambee hiyo kwa
asilimia sita.Picha na IKULU
0 comments:
Post a Comment