Mkurugenzi
wa SONGAS Limited Bw;Christopher Ford(katikati),akimkabidhi mfano wa
hundi yenye thamani ya dolla za kimarekani 10,000, mgeni rasmi wa
harambee hiyo.kushoto meneja rasilimali Songas Bi Agatha Keenja.
Mgeni
rasmi wa harambee hiyo akimpa mkono wa asante mwakilishi wa kampuni ya
Home Shopping Centre Bi Madiha Al Harthy (kushoto),Salma baada ya
kuchangia sh. milioni 22.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja
(katikati) akipongezwa na Mgeni rasmi wa harambe hiyo baada ya
kuchangia sh. 500,000.
Meya
wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto), akimkabidhi mfano wa
hundi yenye thamani ya sh.milioni 10, Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa, aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia mpango wa
elimu Kata ya Kipawa, iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Fedha hizo
zilitolewa na Manispaa hiyo ambapo zaidi ya sh. milioni 400
zilipatikana.
.Diwani wa Kata ya Kipawa Bonah Kaluwa, akitoa neno la shukurani kabla ya kuanza kwa harambee hiyo.
Wadau
mbalimbali wakiwa kwenye harambee hiyo,wakiongozwa na Waziri Mstaafu
Edward Lowassa(wa Pili Kulia) na Meya Wa Ilala Jerry Silaa
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye harambee hiyo
Mbunge
wa Jimbo la Segerea, Dk. Makongoro Mahanga (kulia), Meya wa Manispaa
ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto) na Mwenyeji wa harambee ya kuchangia
mpango wa elimu wa Kata ya Kipawa, Diwani wa Kata hiyo Bonah Kaluwa,
wakimuongoza Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye alikuwa mgeni
rasmi kuingia ukumbini.Picha Zote na Dotto Mwaibale
---
Mbunge wa Jimbo la Segerea Dk.Makongoro Mahanga aliwashukuru wadau waliojitokeza kuchangia kata hiyo ambayo ipo katika jimbo lake na kuwataka wadau wengeni kuchangia kata zingine ili kukabiliana na matatizo hayo katika shule mbalimbali.
---
WAZIRI Mkuu wa zamani , Edward Lowassa, ameendeleza kuwa mstari wa
mbele katika harakati zake za kuchangisha mamilioni ya fedha baada ya
kuchangisha Sh.421,850,000 kwa ajili ya kuboresha Mfuko wa Elimu Kata ya
Kipawa katika Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Lowassa ambaye ni mbunge wa Monduli (CCM), aliendesha harambee hiyo
juzi katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Kempiski Jijini Dar es Salaam
ambapo yeye mwenyewe alichangia Sh.milioni 10.
Katika harambee hiyo miongoni mwa makampuni yaliyochangia kiasi kikubwa
ni Lion Club Sh.milioni 70, Home Shipping Center Sh.milioni 22,
African Barrick Gold Dola 10,000, Songas Dola 10,000, Maersk Sea Line
ilichangia Sh.Miliono 90, na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja
alichangia milioni Sh.10.
Wengine waliochangia ni madiwani, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi,
Chadema, taasisi za watu binafsi na mtu mmoja mmoja ambapo Radio Clauds
walitoa muda wa hewani wa kutangaza mpango huo wenye thamani ya sh.
milioni 12.
Akizungumza kabla ya kuendesha harambee ya kuchangisha, aliwataka
Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuendelea kuwahamasisha
wananchi kuwekeza katika kuchangia sekta ya elimu.
Lowassa alimpongea Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, kwa
jitihada zake alizozionyesha za kuchangia elimu na kuwataka madiwani
wengine kuiga mfano huo.
Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, kwaupande wake alisema shule
saba za Msingi na Sekondari zilizopo kata hiyo zinakabiliwa na matatizo
lukuki ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa hali inayosababisha
wanafunzi kati ya 140 hadi 160 kusomea katika darasa moja.
.
“Shule za kata yangu kwa kweli zinakabiliwa na changamoto nyingi, kwa
mfano Shule ya Msingi ya Majani ya Chai ina vyumba vya madarasa nane
wakati wanafunzi waliopo ni 2,200, Shule ya Msingi ya Minazi Mirefu
madarasa yake yaliyopo ni machakavu pia hayatoshelezi,”alisema Kaluwa.
Kaluwa alisema jitihada nyingine zilizofanywa katika kutafuta pesa kwa
ajili ya kuziboresha shule hizo ambapo Machi 17 mwaka huu kuliitishwa
matembezi ya hisani yaliyoongozwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Aliongeza kuwa katika hafla hiyo kiasi cha shilingi milioni 15
kilichangwa na wadau mbalimbali ambapo kati ya hizo Sh.Milioni 3
zilitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Clouds Media Group
ambao walitoa shilingi milioni moja na wanafunzi kadhaa wa shule za
msingi na sekondari.
Mbunge wa Jimbo la Segerea Dk.Makongoro Mahanga aliwashukuru wadau waliojitokeza kuchangia kata hiyo ambayo ipo katika jimbo lake na kuwataka wadau wengeni kuchangia kata zingine ili kukabiliana na matatizo hayo katika shule mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment