NI UTAMADUNI TULIOJICHAGULIA
Na Deus Valentine
Watanzania wengi bado hatujaweza kutambua uwezo mkubwa tuliokuwa nao katika kuchangia
maendeleo yetu. Inaeleweka kwamba kumekuwa na kilio kikubwa kuhusu michango ya kila siku katika
sekta ya elimu. Hatahivyo mengi ya malalamiko haya yanatokana zaidi na wasiwasi wa matumizi ya
michango husika. Michango hii ikielekezwa mahala stahiki na kuhusisha wachangiaji juu ya matumizi
yake ina uwezo mkubwa sana wa kubadilisha maisha ya watoto wetu walioko mashuleni.
Tatizo sio UWEZO, tatizo hasa ni NIA. Watanzania kwa kiasi kikubwa tumekuwa na utamaduni wa
kuchangia zaidi shughuli zinazoshahabiana na anasa kuliko kuchangia maendeleo. Kwa wenzetu
wakenya kuchangia watoto wa majirani kwenda shule ni sehemu ya utamaduni uliojikita. Mathalani
kwa mkoa wa Dar es Salaam ambapo kuna watanzania zaidi ya milioni nne watu 100,000 huudhuria
sherehe za harusi kwa mwezi kiwango cha chini cha uchangiaji kawaida ni Tshs 60,000. Kama hii
ndiyo hali inamaanisha kuwa kwa mwaka sisi wakazi wa Dar es Salaam tunatumia kiasi cha shillingi
72,000,000,000,000 kiasi ambacho kingeweza kupeleka watoto 720,000 kwa gharama ya Shillingi
100,000 kwa mwaka. Kwahiyo tungetoa asilimia kumi tu ya matumizi yetu kwenye harusi tungepeleka
watoto 72,000 shule kila mwaka!!!
Labda tutaulumu mfumo wetu wa ujamaa kwa kutuzoesha kwamba tungeweza kupata huduma zote
toka serikalini. Serikali ikawa ndio baba ndio mama na hivyo hata wajibu wa kimsingi kama kupata elimu
ya msingi tukaiachia serikali. Umiliki wetu wa jambo hili la msingi na lazima ukapotea kwa utaratibu
huo. Ni rahisi kusema kuwa serikali inakusanya kodi kwahiyo ifanye kila kitu lakini ni sawa na kuomba
rafiki yako amtunze mwanao wakati ukilipia gharama za matunzo hayo. Ni dhahiri bado utahitaji
kuingia gharama za kuhakikisha mwanao anapata matunzo yanayokidhi mahitaji na ndipo hapo kila
mara utakapomtembelea mwanao utajikuta ukiongeza kagharama kidogo ka kununua pipi, kubadili
nepi, kubadili maziwa na vitu vingine vidogo vidogo ambavyo huwa haviachi kuibuka. Bila shaka wote
tukichulia elimu kwa uzito tunaouchukulia watoto wetu wa kuzaa tunaweza kupiga hatua.
Natoa wito kwa kila mmoja wetu kutafakari nafasi yake katika maendeleo ya elimu nchini. Tunaweza
kuendelea kukaa kimya au kuchukua hatua sasa. Nwakaribisha vile vile kuendeleza mjadala kupitia
ukurasa wa faceboo @Educate the Children of Tanzania na kupitia twitter @shujaawakarne.
Mwandishi wa makala haya ni Katibu Mtendaji wa asasi ya EDUCATE THE CHILDREN; asasi ya kitanzania
inayojihusisha na kuchochea upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wa kitanzania na kwa namna ya
pekee watoto wanaotoka kwenye familia duni.

0 comments:
Post a Comment