TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, May 19, 2012

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Mvomero(CCM)Amos Makalla Afanya Ziara Jimboni Kwake

7:01 PM

 Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, wakiwahutubia wakazi wa Kata hiyo na kusisitiza ujenzi wa soko na miundombinu ya visima vya maji kwa wananchi hao.
 Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Nassor Seif ,Rehema  Kapinga  ( kushoto) akipokea seti moja ya Kompyuta yenye thamani za zaidi ya sh: milioni moja ukiwa ni msaada kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, wakati wa mkutano mkuu uliofanyika Mei 16, mwaka huu , eneo la Madizini katika Kata ya Mtibwa.
 Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ( mwenye Kaunda suti) ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, akiangalia hatua za ujenzi wa shule ya sekondari ya watoto wa wafugaji  katika Kijiji cha Wafugaji  cha Mela, Kata ya Melela, Wilayani humo Mei 18, mwaka huu alipofanya ziara ya kuangalia shughuli za maendeleo ambapo aliahidi  kuwaunga mkono kwa  kuwapatia misaada mbalimbali kwa ajili ya ujenzi.
 Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, akioneshwa eneo la ujenzi wa soko la kisasa katika Kijiji cha Mvomero, Kata ya Mvomero , kabla ya kuwahutubia wananchi wa Kata hiyo , Mei 16, mwaka huu.
Baadhi ya akina mama wa jamii ya wafugaji wa Kimasai wa Kijiji cha Mela, Kata ya Melela, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, wakimwimbia nyimbo za kumkaribisha Mbunge wa Jimbo hilo, Amos Makalla ( hayupo pichani) ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo alipofanya ziara yake Mei 18, mwaka huu Kijijini hapo.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA