Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu (aliesimama) akifungua Mkutano wa kwanza wa Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) April 12,2012 jijini Tanga, wenye wajumbe 70. Katika hotuba yake Waziri amesema kwa kutamua umuhimu wa mfanyakazi katika kuongeza tija na Ufanisi wa Mamlaka,wizara inampango endelevu wa mafunzo ,wenye lengo la kukuza Ustadi na Uwezo wa Wafanyakazi katika kumudu mazingira yake ya kikazi, Ili kufikia lengo hili Mamlaka yake hutenga fungu la fedha za mafunzo, zisizoponua asilimia tano ya Bajeti yake ya kwaida ya kila mwaka, hivyo katika mwaka 2012/13 Mamlaka inategemea kutumia sh.1.5 bilioni,
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Fadhili Manongi akimkaribisha Waziri w a Wizara ya Uchukuzi Omari Nundu (hayupo pichani ) kufungua mkutano wa kwanza wa Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Aprili 12,2012 ,jijini Tanga
Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu (kushoto) akiongea na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Usafiri kutoka Wizara ya Uchukuzi Saad Fungafunga (mwenye Kaunda) wakati wa kufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Baraza la wafanyakazi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga jijini Tanga –Apirili 12,2012.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga ambao unafanyika jijini Tanga April 12,2012 na umefunguliwa na Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu (hayupo pichani) wajumbe 70 wanahudhuria.Picha na Mwanakombo Juma
0 comments:
Post a Comment