TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, April 17, 2012

Wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu Dar wafukuzwa

6:06 PM
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimewafukuza wanafunzi wanne kutokana na kudaiwa kuwa vinara wa maandamano yaliyofanyika Novemba 11, 2011 kupinga wenzao waliodahiliwa kujiunga na chuo bila kupewa mikopo.

Wanafunzi waliofukuzwa ni Nduguri Francis, Mabirika Mawazo, Mesaya Ismael na Laizer Yonas.

Barua ya kufukuzwa kwa wanafunzi hao iliyosainiwa na Makamu Mkuu wa Chuo UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala, Machi 20, 2012 inasema hatua hiyo ilifikiwa kwenye kikao cha 207 Januari 10, 201.

Kwa mjibu wa barua hiyo, kufuatia maandamano hayo yaliyosababisha uvunjifu wa amani chuoni hapo na baraza la ushauri limeadhimiria kuwafukuza chuo.

Wanafunzi hao wamepinga hatua hiyo kutokana na taarifa za kufukuzwa  kutofautiana kutoka kwa mshauri wa wananfunzi na barua husika.

Francis alisema Desemba 14, mwaka jana walipewa barua ya kusimamishwa kwa miezi minne kufuatiwa kutuhumiwa kuwa vinara wa maandamano na kuwataka kutoonekana maeneo ya chuo.

Alisema kutokana na kutofautiana kwa barua hiyo na tarehe waliyopewa barua hizo, kuna kitu katikati ambacho kinaonyesha haki kutotendeka kama ambavyo ilitakiwa.

Kufikia sasa, idadi ya wanafunzi waliofukuzwa inakuwa 65 wakati 90 wamesimamishwa kwa uchunguzi zaidi.

taarifa via gazeti Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA