TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, April 2, 2012

Vodacom Tanzania Kupitia Mradi Wake wa MWEI Yawasaidia Kinamama 425 Mkoania Pwani

9:22 AM
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akimkabidhi fedha Mwanaidi Said ambae ni mmoja wa akinamama wajasiliamali wa kikundi cha Kilangalanga cha Mlandizi Mkoani Pwani ,Fedha hizo zilitolewa na Vodacom Tanzania  kupitia mradi wake wa MWEI kwa ajili ya kusaidia wakinamama wajasiliamali na kurudisha mikopo hiyo kwa njia ya m-pesa bila riba. Jumla ya kinamama 425 walinufaika na mkopo huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 30. Katikati ni Meneja mradi huo Mwamvua Mlangwa. 
  Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akimkabidhi fedha Khadija Khalifan ambae ni mmoja wa akinamama wajasiliamali wa kikundi cha Kilangalanga cha Mlandizi Mkoani pwani ,Fedha hizo zilitolewa na Vodacom Tanzania  kupitia mradi wake wa MWEI kwa ajili ya kusaidia wakinamama wajasiriamali na kurudisha mikopo hiyo kwa njia ya m-pesa bila riba. Jumla ya kinamama 425 walinufaika na mkopo huo wenye thamani zaidi ya shilingimilioni 30. Katikati ni Meneja mradi huo Mwamvua Mlangwa na Kuliani Diwani wa kata ya Janga Mlandizi Fedilia Simba.
Meneja wa mradi wa MWEI unaondeshwa na Vodacom Tanzania, Mwamvua Mlangwa,akimkabidhi F edha  Radhia Abdalah, ambazo ni mkopo usio na riba inayotolewa na kampuni hiyo na kurudishwa kwa njia ya m-pesa,zaidi ya shilingi Milioni 30 zimetolewa kwa vikundi vya kinamama wajasiliamali wa kikundi cha Kilangalanga kilichopo Mlandizi mkoani Pwani,Jumla ya kinamama 425 wamenufaika na mkopo huo
 Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akifafanua jambo kwa wakina mama wajasiliamali wa Mlandizi Mkoani Pwani ,kuhusiana na matumizi ya mikopo waliyopewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wa MWEI,Vodacom kupitia mradi huo umewanufaisha  jumla ya wanawake 425 kwa kuwapa mikopo isiyo na riba wa zaidi ya shilingi Milioni 30 Mkoani Pwani. 
   007.Mratibu wa mradi wa MWEI wa Vodacom Tanzania Mgongo Emmanuel akiongea na wakinamama wajasiliamali wa vikundi mbalimbali kutoka katika kijiji cha Kilangalanga cha Mlandizi kabla ya kuanza kuwakabidhi mikopo yao isiyo na riba kwa ajili ya kuendeleza biashara zao na kurudisha mikopo hiyo kwa njia ya m-pesa,jumla ya kinamama 425 walinufaika na mkopo huo wa zaidi ya shilingi Milioni 30.
Baadhi ya akina mama wajasiliamali wa kikundi cha Kilangalanga kilichopo Mlanzidi mkoani Pwani ,wakifurahia kupata mikopo isiyo na riba kutoka Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa MWEI.Jumla ya kinamama 425 wamenufaika na mkopo huo wa zaidi ya shilingi milioni 30.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA