Balozi mdogo wa Rwanda nchini Tanzania Mh. Sano Lambert (katikati) akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 18 ya mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994. Katika Ujumbe wake ameitaka Jamii ya Wanarwanda na Dunia kwa ujumla kuchukulia tukio hilo kama changamoto ya kudumisha amani na upendo duniani na kutaka Mataifa duniani kote kuishi bila itikadi za Kikabila. Kulia ni Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Stella Vuzo na kushoto ni First Secretary wa Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania Bw. Ernest Bugingo.
Pia ametumia fursa hiyo kuialika jamii nzima ya Watanzania na wageni waliopo hapa nchini kuhudhuria mkusanyiko utakaofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tarehe 7 mwezi huu wenye lengo la kuzungumzia sababu zilizopelekea kutokea mauaji hayo ya Kimbari, madhara yake, na nini kifanyike ili kuhakikisha matukio kama hayo yahatokei tena si tu Rwanda bali katika Mataifa yote Afrika na Duniani kwa Ujumla. Katika siku hiyo kutakuwa na mashairi, ngonjera, filamu fupi na ushuhuda kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wahanga na walioshuhudia mauaji hayo.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni "Let’s learn from our history to shape a bright future".
|
0 comments:
Post a Comment