TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, April 17, 2012

Sudan yatangaza uadui na Sudan Kusini

1:28 PM
Bunge la Sudan limepiga kura na kuitangaza Sudan Kusini kuwa adui wa nchi hiyo, ni baada ya majeshi ya Sudan Kusini wiki iliyopita kutwaa eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta.

Spika wa bunge la Sudan, amesema nchi yake itatumia kila raslimali iliyonayo kupambana na Sudan Kusini.
Shambulio la Jumanne wiki iliyopita katika eneo la mafuta la Heglig, lenye umuhimu mkubwa kwa uchumi wa Sudan Khartoum, limesababisha kufungwa kwa shughuli za uzalishaji wa mafuta.
Afisa wa Sudan katika ubalozi wa Sudan mjini London, Dr Kalid Mubarak, ameiambia BBC kuwa sio nchi yake pekee inayolaani vitendo vya Sudan Kusini.
Afisa huyo anasema jamii yote ya kimataifa inailaumu Sudan Kusini kwa uchokozi wake.
Sudan kusini imekuwa ikiilaumu Sudan kwa kushambulia maeneo yake.
Mwandishi wa BBC aliye Khartoum James Copnall anasema kuwa kufuatia tangazo hilo kuna hatari ya nchi hizo mbili kuingia katika vita.
Hatua ya bunge la Sudan ya kupiga kura ya kuitangaza Sudan Kusini kama adui inakuja wakati msemaji wa umoja wa mataifa akithibitisha kuwa ndege za Sudan zimekuwa zikishambulia kambi za maaskari wa kulinda amani zilizoko maeno ya Sudan Kusini. BBC

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA