TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, April 23, 2012

MAPENDEKEZO YA BAJETI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA YAONGEZEKA KWA ASILIMIA 12.6.

3:55 PM

Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida Higa Mnyawi akitoa taarifa yake ya mapendekezo ya bajeti kwa mwaka ujao wa fedha mbele ya kikao cha madiwani.
Baadhi wa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Singida wakifuatilia kwa makini mapendekezo ya bajeti ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha ujao, yaliyokuwa yakiwasilishwa na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Higa Mnyawi (hayupo kwenye picha).Picha zote na Nathaniel Limu
---
Na Nathaniel Limu.
Halmashauri ya wilaya ya Singida inatarajia kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 30.4 kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato katika kipindi cha mwaka wa fedha unaoanza Julai mwaka huu hadi Juni mwakani.

Akitoa taarifa ya mapendekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/2013 mbele ya kikao cha madiwani cha bajeti, Makamu Mwenyekiti wa  halmashauri hiyo Higa Mnyawi, amesema fedha hizo za bajeti  ni kwa ajili ya kulipia mishahara, matumizi ya kawaida (oc)  na kugharamiwa miradi ya maendeleo ya wananchi.

Mnyawi ambaye ni diwani wa kata ya Ikhanoda, amesema bajeti hiyo imeongezeka kwa shilingi 4,550,253,521 ambayo ni sawa na asilimia 12.6 ikilinganishwa na shilingi 25,899,370,000 bajeti ya 2012/2013.

 Akifafanua zaidi, amesema wanatarajia kupokea ruzuku kutoka serikali kuu ya shilingi 19,641,094,712 kwa ajili ya kulipaa mishahara.
Aidha, Makamu Mwenyekiti huyo amesema  pia serikali kuu itawapatia ruzuku ya shilingi 3,85,893,000 kwa ajili ya kugharamia matumizi ya kawaida (oc), shilingi 5,957,827,805, kwa ajili ya miradi ya maendeleo na shilingi 1,004,817,000 zitatokana na  mapato ya vyanzo vya ndani ya halmashauri.

 Mnyawi amesema wadau wa maendeleo ya halmashauri hiyo katika uandaaji wa mipango wa bajeti hiyo, wameendelea kuzingatia mfumo wa fursa na vikwazo vya maendeleo (O&OD).

Wakati huo huo, makamu wenyekiti huyo, alitumia fursa ya hiyo kwa niaba ya uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Singida, kutoa shukrani za dhati kwa serikali kuu, kwa kuwawezesha  fedha pamoja na ushauri nasaha katika kuboresha utekelezaji wa majukumu mbalimbali.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA