TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, April 30, 2012

Mamlaka ya hali ya hewa yatoa tahadhari ya uwezekano wa mvua kubwa

4:53 PM
Taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ya kumbukumbu namba: 20120430-02 iliyotolewa saa 2:00 Asubuhi (saa za Afrika Mashariki) inatahadharisha uwezekano wa kuwepo kwa mvua kubwa kuanzia tarehe 30 Aprili 2012 mpaka tarehe 04 Mei 2012.

Inatarajiwa kuwepo mvua kubwa (zaidi ya milimita 50 katika kipindi cha saa 24 kila siku) katika baadhi ya maeneo yaliyotajwa hapo chini. Kiwango cha uhakika ni 80%.

Maeneo ya kuzingatia: Mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Tanga, Morogoro, Pwani na visiwa vya Unguja na Pemba.

Angalizo: Wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa Bahari na nchi kavu, wanashauriwa kuchukua tahadhari. Aidha taasisi zinazohusika na Maafa zinashauriwa kuchukua hatua stahiki.

Maelezo ya ziada: Mamlaka inaendelea  kufuatilia mifumo ya hali ya hewa na kutoa taarifa kila itakapobidi.

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2012/04/mamlaka-ya-hali-ya-hewa-yatoa-tahadhari-ya-uwezekano-wa-mvua-kubwa.html?utm_source=feedburner&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+wavuti+%28Wavuti+%29#ixzz1tWQ3jze5

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA