TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, April 11, 2012

LULU APANDISHWA KIZIMBANI LEO KUJIBU TUHUMA ZA MAUAJI YA KANUMBA

6:23 PM
MUIGIZAJI wa Filamu nchini anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie,Marehemu Steven Kanumba, Elizabeth Michael almaarufu LULU,leo  amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka yanayomkabili kuhusu kuhusika kwake na kifo cha Muigizaji huyo nguli kilichotokea usiku wa kuamkia jumamosi iliyopita.

Elizabeth Michael amesomewa mashtaka hayo ya mauaji ya Muigizaji wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda.

Elizabeth alielezwa kuwa hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena Aprili 23 mwaka huu.

Muigizaji huyo aliwasili mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi kama mshale na kwa ulinzi mkali na pia ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba hakuna hata mwandishi aliyeweza kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye tuhuma za mauaji Na kupandishwa katika gari ndogo nyeupe aina ya Suzuki Grand Vitara yenye namba za usajiri T 848 BNV huku kwenye kioo nambari zake zikisomeka PT 2565.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA