TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, April 18, 2012

KAMPUNI YA BIA TBL YATOA SH. MIL. 100 KUSAIDIA UJENZI WA CHUO KIKUU TUMAINI JIJINI DAR ES SALAAM

9:21 AM


Michoro ya majengo mbalimbali ya chuo hicho yatakayojengwa eneo la Mwenge, Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ushauri wa ujenzi wa majengo hayo, Nosuto Associated, Thomas Kalugula akielezea jinsi ujenzi wa majengo hayo utakavyofanyika.
Mkuu wa Kikuu cha Tumaini, Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa,  Profesa Geoffrey Mmari (katikati) akielezea mikakati ya ujenzi wa majengo mapya ya chuo hicho. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo ambayo imetoa msaada wa sh. milioni 100 za
kusaidia ujenzi wa majengo hayo.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo(kushoto),akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Huduma za Jamii waKanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Robert Charles (kulia) mfano wahundi yenye thamani ya sh. mil. 100 za kusaidia ujenzi wa majengo mapya ya Chuo Kikuu cha Tumaini, Dar es Salaam. Anayeshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, ni Mkuu wa chuo hicho kamapasi ya Dar es Salaam, Profesa Geofrey Mmari.
Baadhi ya wakufunzi na wafanyakazi wa chuo hicho.
Naibu Katibu Mkuu Huduma za Jamii wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Robert Charles (kulia) akimshukuru Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto) mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 100 za kusaidia ujenzi wa majengo mapya ya Chuo Kikuu cha Tumaini, Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Geoffrey Mmari.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA