![]() |
| KIUNGO wa Chelsea, Frank Lampard amewapongeza wachezaji wenzake baada ya Chelsea kutoka nyuma mbele ya Barcelona na kushinda kwa jumla ya mabao 3-2 na kutinga Fainali ya Ligi ya Mabingwa. The Blues walikuwa nyuma kwa mabao 2-0 katika usiku huu kabla ya kumpoteza nahodha wake, John Terry aliyetolewa kwa kadi nyekundu kwa kumpiga teke Alexis Sanchez. Lakini bao la kushitukiza la Ramires kabla ya mapumziko lilirejesha matumaini kwa Chelsea kabla ya Lionel Messi kukosa penalti na makosa ya safu ya ulinzi yakampa mwanya Fernando Torres kutimka kwa kasi kwenda kufunga bao lililokamilisha bei ya tiketi ya Chelsea kwenda Munich dakika ya mwisho mchezo. “Nini kiwango! Najua ngoma ilikwishakuwa ngumu wakati huo, lakini tulipigana hadi mwisho sana," alisema Lampard. “Najua watu walitaka kuona soka maridadi, lakini tukiwa 10 kwa dakika 50 zilizosalia na tukiwa nyuma kwa mabao mawili na kucheza namna ile- tulionyesha morali ya aina gani - ngumu kuamini tulivyoshughulika! “Saa zilikuwa kama zinakwenda taratibu sana kipindi cha pili, lakini nilikuwa na fikra utakuwa usiku wetu. Wote mnafahamu wanaweza kufunga wakati wowote kwa sababu ya wachezaji wao walionao kwenye timu, lakini kulikuwa kuna kujituma juu yetu. “Katika mchezo unaopata kile unachostahili na tulikuwa wote wamoja na tulipigana na matunda yake ni matokeo mazuri tuliyopata.” Lampard alisema... Soma zaidi...htttp://www.bongostaz.blogspot.com |
Wednesday, April 25, 2012

0 comments:
Post a Comment