TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, March 5, 2012

Rais Jakaya Kikwete Atua Mkoani Kilimanjaro Kwa Ziara Ya Kikazi Ya Siku Tatu

9:17 AM

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokewa kwa furaha   walipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)jana jioni tayari kwa ziara ya siku tatu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa kwa furaha mara alipotua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jioni Jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea taaria ya Mkoa toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama mara tu baada ya kuwasili Ikulu ndogo mjini Moshi Jana Jioni.Picha na IKULU
------
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Moshi  jana, Jumapili, Machi 4, 2012 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.Miongoni mwa shughuli ambazo Mheshimiwa Rais atafanya ni pamoja na kuzindua kampeni ya kupinga ukatili na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake ambayo ataizindua kwa kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro iliyopewa jina la “Kilimanjaro Speak Out, Climb Up”.

Shughuli hiyo itakayofanyika kesho Jumatatu, Machi 5, 2012 asubuhi, imepangwa kwenye Lango la Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)Mbali na kuanzisha kampeni hiyo, Mhe Rais pia atafungua Mkutano wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika kwenye Chuo cha Polisi mjini Moshi.
Hii ni ziara ya kwanza ya Mhe Rais Kikwete katika Mkoa wa Kilimanjaro tokea alipotembelea Mkoa huo wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

MWISHO

Imetolewa na 

KURUGENZI YA MAWASILINO YA RAIS
MARCH 4, 2012
MOSHI

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA