TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Sunday, February 26, 2012

Uchambuzi Wa Habari: Gazeti Uhuru Linapofichua Njama Za Kufunika Madudu Ya Ekelege Wa TBS!

10:00 PM
Mhariri wa gazeti la Uhuru anaitwa Jaqueline Liana.  Hakika anastahili
pongezi kwa kazi yake njema kwa  taifa. Niweke wazi, katika magazeti
yote niliyoyapitia siku ya jana Jumamosi, gazeti la Uhuru ndilo kwangu
lilitia fora.


Kati ya habari kadhaa  zenye kumfumbua macho msomaji, gazeti Uhuru
lilibeba habari tatu zenye umuhimu mkubwa kwa nchi yetu; habari kuu
ilikuwa na kichwa cha habari; “ Ripoti uozo TBS yavaiva- Njama za
kuizima zaandaliwa”. Nyingine ni; “ Majengo ya UDA kuhifadhi
makontena”. Na mwisho ni wito; “Tumieni mitandao ya kijamii
kuhabarisha”. Habari hizo mbili za mwisho nitazichambua katika siku za
usoni kutokana na ufinyu wa muda kwa sasa.


Nianze basi  na habari kuu iliyotokana na uchunguzi wa gazeti Uhuru;
Mwandishi anabainisha, kuwa taarifa ya uozo wa ndani ya Shirika la
Viwango Tanzania  ( TBS) imekamilika na imewasilishwa  kwa Spika wa
Bunge kwa hatua zaidi.

Kwamba wakati  ripoti hiyo ikiwa tayari na huku Watanzania wakisubiri
hatua gani zitachukuliwa, gazeti Uhuru limebaini uwepo wa mipango
kabambe inayosukwa ili  kuzima na kuwalinda  vigogo wa shirika hilo la
umma wanaotuhumiwa  kufanya mambo kinyume na taratibu.


Uhuru linabainisha, kuwa Kamati  ya Bunge ya Mahesabu ya Mashirika ya
Umma  ( POAC) imebaini matatizo mengi ndani ya TBS  yakiwemo ukaguzi
wa bidhaa usiokidhi viwango na mazingira  ya rushwa miongoni mwa
maofisa waandamizi.  Na kutokana na kubainika kwa madudu hayo, Kamati
hiyo  imependekeza  baadhi ya maofisa waandamizi wa TBS, akiwemo
Mkurugenzi Mkuu, Charles Ekelege, wasimamishwe kazi kupisha uchunguzi
wa tuhuma zinazowakabili.


Na licha ya Kamati ya Bunge kukamilisha ripoti yake hiyo, uchunguzi
uliofanywa na  gazeti la Uhuru  unaonyesha kuwa kuna mipango inasukwa
kwa kuwahusisha baadhi ya wabunge, ofisi ya bunge na wizara ya Viwanda
na Biashara  kuhakikisha suala hilo halifikishwi katika mkutano ujao
wa bunge na kuchukuliwa hatua.


Uchunguzi wa  gazeti Uhuru  unazidi  kuonyesha , kuwa  wahusika wa
mpango  huo ni baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe  wa Kamati ya Bunge
ya Hesabu za Serikali ( PAC) na maofisa wa bunge  kwa kushirikiana na
maofisa  waandamizi wa wizara.


Kwa mujibu wa gazeti Uhuru, mmoja wa  wajumbe wa POAC alithibitisha
kuwepo  mipango hiyo  na kuongeza kuwa, baadhi ya wabunge wanatumiwa
katika suala hilo.

Mjumbe mwingine wa kamati hiyo alisema, kwa uozo ndani ya TBS uko wazi
kwa sababu hata wafanyakazi  wa chini wamekuwa wakilalamika  kuwa
wanakwamishwa kufanya kazi ipasavyo na viongozi wao.


” Wafanyakazi  walitueleza kuwa wanapogundua  kuna bidhaa mbovu na
kuzizuia, wafanyabiashara wanazungumza moja kwa moja  na viongozi wa
juu  wa shirika na matokeo yake bidhaa zile ambazo ni mbovu
zinaruhusiwa kutumika.

” Kama watu walioaminiwa na kupewa nafasi kuongoza shirika kubwa kama
hili wanakiuka utaratibu, kuna imani gani tena? Hii inaonyesha watu
hawa  hawana  nia njema  na maisha yetu na wako tayari kuwaangamiza
Watanzania kwa sababu  ya maslahi yao”. Alisema mjumbe huyo.


Kwa mujibu wa gazeti Uhuru,  Makamu wa Mwenyekiti wa kamati hiyo ya
bunge ,  Mbunge wa Ludewa , Deo Filikunjombe, ameweka  bayana msimamo
wa kamati yake, kuwa hawatakubali  suala hilo kuzimwa au kumalizwa
kinyemela kwa sababu  kufanya hivyo  ni kukubali  Watanzania
waendelee kuangamia kwa kutumia bidhaa mbovu.


Filikunjombe anasema;


” Upo ushahidi  kwamba zipo bidhaa zisizo na  viwango kama kondomu,
mafuta ya kupikia, matairi, vyakula na blue band ambazo zina nembo ya
TBS na zinatumika. Huu ni uoza mkubwa, ni lazima tufike  mahali tuseme
basi. Ni lazima TBS isafishwe na wahusika wa mchezo huu mchafu lazima
waondolewe haraka”. ( Deo Filikunjombe, Uhuru Februari 25, 2012)


Naam, kila Mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi yake  hana budi
kuwaunga  mkono wahariri wa mfano wa Jacqueiline Liana na wabunge wa
mfano wa Deo Filikunjombe. Ni Watanzania wenzetu  walioonyesha
utayari wa kujitoa muhanga  kuipigania nchi yao dhidi ya vitendo vya
kifisadi kama hiki cha TBS chenye hatari ya kuliangamiza taifa.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA