TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, February 22, 2012

Maonyesho ya kila mwaka ya kibiashara ya Harusi sasa yaingia mwaka wake wa tatu

10:21 PM
A model during Harusi Trade Fair 2011
 model during Harusi Trade Fair 2011
 model during Harusi Trade Fair 2011 

Maonyesho ya kipekee ya kibiashara ya Harusi Tanzania

Wito kwa wadau wa sekta ya maswala ya Harusi.

Maonyesho ya biashara ya harusi sasa  ni maonyesho makubwa ya harusi nchini yanayojumuisha wadau mbalimbali katika sekta ya harusi kutoka sehemu mbalimbali nchini  Tanzania kwa kuonyesha bidhaa zao na huduma kwa umma kwa ujumla.

“Ndoa ni moja kati ya nyakati za muhimu katika maisha ya binaadamu na sherehe za harusi ni moja kati ya nyakati chache  zinazoleta  marafiki, familia na jamii kwa ujumla  wote kuwa pamoja. Hivyo bila ya msaada kutoka kwa wadau wa sekta ya mambo ya harusi  utambuzi wa kuwa na ndoto ya Harusi bora haiwi yakinifu. Najivunia  katika kutimiza ndoto kugeuka katika ukweli ”. Alisema mwanzilishi wa Harusi Trade Fair Mustafa Hassanali.

Katika mwaka wake wa tatu sasa, Maonyesho ya Biashara ya Harusi yatakuwa na mambo makuu matatu ,ambayo ni  maonyesho yenyewe, majadiliano na maonyesho ya mavazi. Maonyesho yote yatakusanya zaidi ya wafanyamaonyesho 50 ambao watakuwa wakionyesha bidhaa zao na huduma, kwenye Majadiliano kutakua na wageni kadhaa ambao watakua ni wasemaji  katika uwanja wao wa utaalamu , na kuzungumzia mambo yonayohitajika na yasioitajika  na mambo yote yanayohusu harusi, Maonyesho ya mwaka ya Harusi yatahusisha zaidi ya wabunifu kumi wa mitindo na wamiliki wa maduka ya bidhaa za Harusi ,ambapo bidhaa zao hizo zitaonyeshwa na kuuzwa katika maonyesho ya mavazi ya Harusi ambayo yatafanyika tarehe 31 Machi- 2012 kuanzia saa 2 Usiku nakuendelea.

“Mwaka jana tulikua na wageni  zaidi ya 1500 ambao walihudhuria maonyesho haya, tunatarajia wageni zaidi mwaka huu . Kuvuna faida za matumizi na sehemu pana na masoko ya karibu zaidi, tunawaomba wachuuzi wote wa mambo ya  harusi kuchukua fursa hii ya kila mwaka ya kuonyesha katika maonyesho haya ya  kipekee ya harusi nchini "Alisema Meneja wa Masoko wa Harusi Trade Fair  Hamis K Omary .

Hadi sasa zaidi ya washiriki  18 wa maonyesho ya Harusi  tayari wamedhibitisha kushirki,miongni mwao ni  EndePa event planners, Mkoma Bay lodge iliyopo Pangani, kearsleys travel, Binti Afrika, Wedding Bells, Rose fashion designs, Blind Tiger, MH Gallery, Dia’s , Green Chef na cocktails, GRM production, Pure Beauty , Lotus Creative concepts ,kwa kutaja chache tu.

Harusi Trade Fair 2012 itafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee kwa siku 3 mfululizo kuanzia tarehe 30 marchi- 1 Aprili  kuanzia saa 4:00 asubuhi nakuendelea.

“ Tukiwa tunamalengo makubwa sana ya kutangaza  Harusi Trade Fair na kuitangaza Tanzania kama  mahali  pa Harusi na kama sehemu ya kupumzikia kwa maharusi duniani, ningependa kuwashukuru washirika wetu wote kwa kutuunga mkono kwa miaka yote iliyopita na kuendelea kuomba mashirika na kampuni mbalimbali kutuunga mkono kwa kudhamini Harusi Trade Fair 2012’’ . Almalizia Afisa Mahusiano, Amisa Juma

Harusi Trade Fair 2012 imedhaminiwa na  Clouds Media group, Global Outdoor Systems. H.Models and 361 Degrees

Kwa Mhariri.

Maonyesho ya Harusi, yamefanyika kwenye  ukumbi wa Diamond Jubilee, ukanda wa pwani wa Afrika Mashariki, Dar es salaam Tanzania.

Harusi ni neno la Kiswahili linalosomama katika maana ya kuwaleta pamoja wawili wa jinsia mbili tofauti katika maisha ya pamoja kama mke na mume. Ni wazo la mbunifu wa mavazi Mustafa Hassanali katika mwaka wa 2009 kuwa na maonyesho makubwa kama haya ya Harusi.

Ni maonyesho yanayofanyika mara moja kwa mwaka huku yakiwafikia takriban watu 10,000 wanaotarajia kufunga ndoa, familia na marafiki zao, ambao kwa namna moja au nyingine wanahusika katika maandalizi ya Harusi, huku maonyesho haya yakiwaleta pamoja wahusika na wataalamu wa mambo ya Harusi katika soko moja la siku tatu


Kwa Maelezo zaidi tembelea www.harusitradefair.com

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA