TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, October 13, 2011

Mutassim Gaddafi 'akamatwa' mjini Sirte

2:14 PM
Kumekuwa na taarifa za kuhitilafiana kuhusu mmoja wa wanawe Kanali Gaddafi, Muttasim, ambaye alihudumu kama mshauri mkuu wa usalama wa kitaifa katika serikali ya babake.

Afisa mmoja wa baraza la mpito la kitaifa (NTC) amesema kuwa Mutassim Gaddafi amekamatwa mjini Sirte na kupelekwa Benghazi japo mwngine kutoka baraza hilo hilo amesema kuwa habari hizo haziwezi kuthibitishwa.

Taarifa zinadai kuwa Mutassim alikamtwa akiwa kwenye harakati za kutoroka kutoka mjini Sirte ambao umeshuhudia mapigano makali kati ya wanajeshi wa NTC na wale watiifu kwa Kanali Gaddafi.

Lakini licha ya hilo raia wa Libya mjini Benghazi na hata Tripoli wamekuwa wakisherekea.

Wakuu wa jeshi la NTC wanasema sasa hivi wanadhiti eneo kubwa la mji huo wa Sirte.
Ikiwa kweli Mutassim Gaddafi atakuwa amekamatwa, hii itakuwa habri njema kwa baraza la mpito na pigo kwa makundi yaliosalia yanayo mtii kanali Gaddafi.
Inadaiwa kuwa wanajeshi waliokuwa wakipigana na wale wa baraza la NTC mjini Sirte alipozaliwa Kanali Gaddafi wamekuwa wakimlinda Mutassim.
Ikiwe ni kweli amekamatwa, Mutassim atakuwa wa mtu wa kwanza wa wa jamaa ya Gaddafi kushikwa.
Mke wa kanali Gaddafi na watoto wake wakike wapo nchini Algeria na kaka yake Saif al Islam anadaiwa kuwa mafichoni mjini Bani Walid.
Raia wengi wa Libya wanaounga mapinduzi haya wanahamu kuona kanali Gaddafi ameshikwa akiwa hai.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA