TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, October 24, 2011

MISS JESTINA BLOG YASHINDA TUZO YA BLOG YA MWAKA UK.

12:07 PM

Urban Pulse Creative inapenda Kumpongeza dada yetu Jestina George kwa kushinda tuzo muhimu ya Blog ya Mwaka  katika  tuzo za BEFFTA zilizizofanyika Jumamosi tarehe 22 Octoba 2011 ndani ya ukumbi wa Lighthouse, Camberwell jijini London.
 
Wakati akitoa Hotuba yake Jestina alianza kwa kumshuru Mungu ambae amemwezesha kumpatia uzima, afya njema pamoja na mafanikio  makubwa aliyopata mwaka huu.  Aliendelea kwa kuwashukuru Wazazi wake na mwisho wadau wote ambao walimpigia kura Pia Mabloggers na Tovuti mbalimbali ambazo zimemsaidia kumpigia debe na kuibuka mshindi wa BLOG OF THE YEAR 2011 kutoka kwenye kundi lenye Blog 15 za kimataifa. Hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa Mtanzania kuingia, kushinda na kumfanya kuwa Mtanzania wa Kwanza kupokea tuzo za BEFFTA  kwa upande wa Blogs
 Jestina George ameitoa wakfu Tuzo yake kwa dada yake mpendwa Kissa George ambaye hatunaye tena hapa Duniani.
 Vazi lake lilibuniwa na KIKI wa Kiki's Fashion Tanzania. Kwa maelezo zaidi na taswira mbalimbali za tukio hili Tembelea http://missjestinageorge.blogspot.com/
 
Asanteni,
 Urban Pulse Creative

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA