TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, October 3, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-33

3:37 PM
Wakati tupo na akina Maua na Maneno, mara tukapata taarifa kuwa huko nchi ya jirani kuna jambo limetokea, ni muhimu turejee huko haraka iwezekanavyo, kwahiyo tukatishe kidogo twende na labda tukirudii huku tutakuwa katika kuhitimisha. Karibuni sana.

Tukumbuke kuwa Sweetie alikutwa bafuni kazimia, na Rose akawa kachanganyikiwa kabisa, kwani jinsi livyomuona pale sakafuni, alikuwa kama mfu, ikabidi aanze kazi yake ya udakitari ya huduma ya kwanza, na alipoona imeshindikana, ikibidi atafute msaada na harakaharaka kwa kuonana na wahudumu wa hoteli ambapo kulikuwa na gari la dharura kama hiyo , na mara moja akakimbizwa hospitalini.

Wakati yupo hospitalini Rose alikuwa akiwaza ni nini hasa kimemtokea Sweetie wake, huenda ni kwasababu ya tukio la jana, …tukio la jana, ooh,. Alipofika hapo akatabasamu, na kuanza kupitisha kidole taratibu kwenye sehemu ya mbele ya mdomo wake, na alipohisi msisimuko akaondoa haraka, na kutamani kukasirika, lakini badala yake akatabasamu…mmh, hisia… halafu akatabasamu tena, na kuinuka pale alipokuwa amekaa, na kuwaza ina maana baada ya tukio la jana, hisia zake zimeanza kurudi, chuki kwa wanaume imeondoka…au kwasababu ya kupenda….mmh, kupenda, kumpenda nani…hapana sijapenda, sitaki kupenda, …mmh, lakini najidanganya…na hapo akawaza kwa tukio la jana, akianzia pale alipoamuka asubuhi.bofya hapa

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA