TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, September 27, 2011

HALI MBAYA MBEYA, WAPIGA NONDO WAMWUA POLISI

11:23 PM

Na Gordon Kalulunga, Mbeya.

Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya limedhihirisha wazi kushindwa kuwadhibiti wahalifu wa "upigaji nondo" ambao jana walifanikiwa kumuua PC Meshack (28) mwenye namba G.2795 aliyeuawa majira ya saa 5.15 usiku maeneo ya mabatini.

Kuuawa kwa askari polisi huyo kulifuatia tukio jingine kama hilo ambapo, WP Hawa  ambaye ni mahutiti na amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya baada ya kupigwa  nondo maeneo ya Meta majira ya saa 4.00 usiku. Hawa ni askari wa usalama wa barabarani.

Kabla ya askari polisi hao wawili kupigwa nondo na mmoja kuuawa tukio la kwanza la upigaji nondo na kushambulia mwilini alipigwa, WP Flora aliyepigwa maeneo ya Uyole ambako katika tukio hilo, Richard Shitambala aliuawa.

Mfululizo wa matukiio hayo ya upigaji nondo tayari wahalifu hao wamewaumiza wananchi zaidi ya 20 kwa kipindi cha miezi miwili ambapo katika tukio la jana pekee watu tisa walifikishwa katika Hospitali ya rufaa ya Mbeya wakiwa wamejeruhiwa vibaya.

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo, Mganga wa idara ya wagonjwa wa nje na huduma ya haraka Dk. Dominic Chalu alisema kuwa majeruhi tisa walifikishwa usiku wa kuamkia jana ambapo majeruhi wanne waliruhusiwa kurudi nyumbani, "Tulipokea majeruhi tisa ambapo wanne waliruhusiwa kurudi nyumbani na wengine watano bado wamelazwa na wanaendelea kupata matibabu’’ alisema Dr.Chalu.

Kwa upande wake majeruhi John Komba (38) ambaye ni dereva wa kampuni ya usafirishaji ya Sumry, akiwa kitandani hospitalini hapo alisema kuwa alitoka stendi kuu ya mabasi ya mkoa wa Mbeya akielekea nyumbani kwake alipofika eneo la Forest akiwa nsani ya gari ndogo alisimamishwa na watu watatu waliokuwa wamevalia makoti kisha kumpiga, "Nilipotoka Stendi kuu na kufika eneo la Foresti nikakutana na watu watatu waliokuwa wamevalia makoti marefu na niliposimama wakajitambulisha kuwa wao ni askari polisi na kuniamuru nizime taa kisha wakanishambulia na nondo mara tatu kichwani na nikapoteza fahamu’ ’alisema kwa shida Komba huku akionekana kuwa na maumivu makali.

Naye majeruhi Adam Juma alisema kuwa anakumbuka ilikuwa majira ya saa tatu usiku akiwa katika mtaa wa Mbalizi Road eneo kata ya Mbatini Jijini Mbeya alishambuliwa na watu ambao hawakumbuki kisha akapoteza fahamu.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na blogu ya Kalulunga.blogspot.com waliofika kuwaona majeruhi hao katika Hospitali ya rufaa ya Mbeya kwa ombi la kutoandikwa majina yao walisema kuwa Jeshi la polisi mkoani hapa linapaswa kujipanga na kuondoa mlundikano wa Trafiki barabarani badala yake waimarishe doria za wahalifu wakiwemo wapiga nondo, "Utakuta kituo kimoja kina askari wanne mpaka watano mchana huku wakipokea elfu moja moja kwa madereva na makondakta wao! Hivyo umefika wakati kupunguza trafiki hao kujazana kila baada ya vituo viwili barabarani mchana badala yake wapangwe kwenye doria ili kuondoa hali hii’’ walisema wananchi hao wakiwemo waliokuwa wakiuguza ndugu zao.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo likiwemo la kifo cha askari wake.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA