Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Shirika la Oikocredit Tanzania
limezikopesha Saccos tatu za Mwanza, Musoma na Shinyanga Foundation
Fund jumla ya milioni 700/- zitakazotumika kusaidia wanachama wa taasisi
hizo kujikomboa na umasikini unaowakabili na hatimaye kujiletea
maendeleo katika jamii zao.
Katika
makabidhiano hayo yaliyofanyika jijini Mwanza hivi karibuni Saccos ya
Mwanza imekopeshwa jumla ya milioni 350/-, Musoma Sacco milioni 200/- na
ile ya Shinyanga Foundation Fund shilingi milioni 150/-.
Akikabidhi
msaada huo Meneja wa Oikocredit Tanzania Deus Manyenye amesema kwa
taasisi nyingi za kifedha haziamini kusaidia kwenye miradi ya watu
masikini taasisi yake imejikita kukopesha miradi yenye manufaa kwa jamii
hususani ile inayojumuisha ngazi ya madaraka kwa wanawake.
“Oikocredit
hupendelea mno miradi ambayo wanawake wanajumuishwa kwenye ngazi za
maamuzi. Sisi tunaamini kwamba watu masikini wanaweza kujijengea maisha
mazuri wakipewa fursa kama kuwezeshwa kifedha,” alisema Manyenye.
Akifafanua
Meneja huyo amesema, tangu Oikocredit ianzishwe nchini mwaka 2006
tayari wameshakopesha miradi 30 yenye thamani ya shilingi bilioni 30 ili
kuwasaidia watu masikini na wasiojiweza wanaoishi mijini na vijijini.
Takwimu zilizotolewa na shirika hilo
ni kwamba inakadiliwa watu zaidi ya Bilioni 1.5 duniani wanaishi kwenye
umasikini. Hawa siyo kwamba hawana uwezo, ila wanakosa fursa za kupata
hela na kujikwamua, alisema Manyenye.
Akizungumza
kwa niaba ya wenyeviti wa Saccos zilizokopeshwa fedha hizo, Mwenyekiti
wa Shinyanga Foundation Fund, Paulo Sangija alisema watatumia fedha hizo
kwa wakati ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa ya kuikomboa jamii
kuondokana na umasikini.
“Mkopo
huu umefungua mlango wa pili, tutakachohakikisha sisi ni jamii
inanufaika na fedha hizi kwani tukizifuja tutadidimia zaidi. Ukikosa
uwezo vilevile mbinu za upatikanaji wa mikopo unakosekana, tunashukuru
na hatutakuangusha,” alisema Sangija.
Mbali na hayo Oikocredit ilishazikopesha jumla ya shilingi bilioni 2.1/- YWCA
Moshi na Saccos ya Wazalendo ili zitumike kuiwezesha jamii ya watu wa
kipato cha chini. Fedha zilizotolewa zilitumika kwa ajili ya ukarabati
wa jengo la makao makuu ya YWCA Moshi na uwezeshaji jamii ili
ijiendeleze kimaisha kupitia Wazalendo.
Shirika hilo
lenye makao yake makuu nchini Uholanzi zaidi ya miaka 36 sasa mapa
kufikia Septemba 2009 limekopesha miradi zaidi ya 780 duniani na hutoa
misaada ya kifedha kwa taasisi ambazo zina mikopo.
0 comments:
Post a Comment