| Wanafunzi wa Shule ya Mtakuja Sekondari School katika picha ya Pamoja. |
| Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Esacs katika picha ya pamoja. |
*NI YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 16
*YASHIRIKISHA SHULE 6 ZA KINONDONI
*WAZAZI WAHIMIZWA KUJITOKEZA KWA WINGI
Na.Mwandishi
wetu
Mashindano
ya mchezo wa soka ya DAR SECONDARY
SCHOOL CUP yanayoshirikisha vijana wa shule za sekondari jijini Dar es
Salaam wenye umri chini ya miaka 16 yamezinduliwa rasmi katika viwanja vya Chuo
Kikuu cha Dar – UDSM.
Mashindano
hayo yameandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Upendo Youth Development
Organization – UYODEO lenye makao
yake makuu huko Kilwa – Masoko.
Akizungumza
na MO BLOG Mjumbe wa Heshima wa UYODEO na Mratibu wa mashindano hayo
Annick Verstraelen amesema lengo kuu la
mashindano hayo ni kuwakutanisha pamoja wanafunzi kutoka shule mbali mbali
chini ya kauli mbiu ya ‘TUCHEZE PAMOJA’
ili waweze kufahamiana, kushiriki michezo pamoja na kujenga uhusiano.
Amefafanua
kuwa mashindano hayo pia yanalenga kutafuta, kukuza na kuvitumia vipaji
miongoni mwa wanafunzi ili waweze kujitambua wakiwa bado katika umri wa kukua.
Mashindano
hayo mwaka huu yamehusisha timu za shule sita (6) kutoka wilaya ya Kinondoni,
lakini ni matarajio ya UYODEO
kupanua wigo ya mashindano hayo na kufanyika pia katika wilaya za Ilala na
Temeke.
Akizungumzia
changamoto wanazokabiliana nazo katika kuandaa na kufanikisha mashindano hayo,
Annick amesema uhaba wa fedha umekuwa ni kikwazo kikubwa kutokana na gharama za
maandalizi kuwa kubwa ikilinganishwa na uwezo wa shirika hilo, hivyo ametoa
wito kwa wadhamini kujitokeza ili kuwezesha mashindano hayo kufanikiwa kwa
kiwango kilichokusudiwa.
Aidha
Annick ametoa wito kwa wazazi kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia mashindano
hayo, ili waweze kujionea nini watoto wao wanafanya uwanjani na kuweza kuwapa
moyo na kuwaunga mkono ili waweze kutimiza malengo yao katika michezo, kwani
michezo ni afya.
Shule
za Sekondari za wilaya ya Kinondoni zinazoshiriki mashindano hayo ni Kinondoni Muslims, Salma Kikwete, Makongo
Sekondari, ESACS, Mtakuja Beach na DIS.
Shule
hizo zimepangwa katika makundi mawili yenye timu tatu kila moja, ambapo kila
shule itapaswa kucheza mechi mbili katika mfumo wa ligi.
Kundi
la kwanza lina timu za shule za Mtakuja
Beach, DIS na Kinondoni Muslim wakati
kundi la pili lina timu za Salma
Kikwete, Makongo na ESACS.
Mechi
za ligi ya mashindano ya DAR SECONDARY
SCHOOL CUP zitafanyika tarehe 30
April na tarehe Mosi Mei 2011.
Kwa
upande wa udhamini makampuni yaliyojitokeza kudhamini kwa namna moja ama
nyingine kuwezesha ufunguzi wa mashindano hayo ni pamoja na Aurora Premium Outlet Security (T) Ltd,
Image Masters, Continental, MO BLOG –More Benefits, PPF na Azam Football Club.
0 comments:
Post a Comment