Taarifa ya habari iliyosomwa saa saba mchana wa leo kupitia TBC , imetamka kuwa, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (?Serikali au Sehemu ya Serikali?) imetoa ripoti kuhusu tiba inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa La Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapila*
al maaruf, "Babu" huko kijijini Samunge, Loliondo wilayani Ngorongoro,
mkoani Arusha na kusema, "dawa hiyo haina madhara kwa binadamu".
Ripoti
hiyo inafuatia utafiti uliofanywa na timu ya wataalamu toka Mamlaka ya
Dawa na Chakula, TFDA, wakishirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa
ya Binaadamu, NIMR, na Kitengo cha Utafiti wa Dawa za Asili cha Chuo
Kikuu cha Dar Es Salaam, kwamba baada ya uchunguzi wa dawa na kipimo
kinachotolewa na "Babu" (kikombe cha Babu) haina madhara kwa binadamu.
Bofya kifute cha play kusikiliza taarifa ya Habari hiyo.*Usahihi wa jina la Mchungaji
Kumekuwapo upotoshaji wa jina la Mchungaji husika. Awali, aliitwa
Mchungaji (mstaafu) Ambilikile Mwasapile. Wengine wakamwita Ambilikile
Mwaisapile. Wapo wanaomwita Ambilikile Mwasapila na wengine wakamwita
Ambikile Masapile. Uongozi wa Kanisa la KKKT umetoa ufafanuzi wa jina
lake halisi na kusema ni Mchungaji (mstaafu) Ambilikile Masapila.
(credit ya ufafanuzi wa jina New Habari)
|
0 comments:
Post a Comment