JUMUIYA YA WATANZANIA JAPANI
Kumekuwa na wasiwasi mkubwa kwa
Watanzania walio na ndugu, jamaa na marafiki nchini Japani juu ya
usalama wao unaotokana na kutokea kwa majanga makubwa ya tetemeko la
ardhi na Tsunami.
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania
Wanaoishi Nchini Japani (Tanzanite Society) kwa kushirikiana na mtandao
wa Watanzania wanaoishi nchini Japani (wanatija), pamoja na ofisi zetu
za ubalozi hapa Japani tunapenda kuchukua fursa kuwataarifu kuwa mpaka
sasa tumeweza kuthibitisha kuwa karibu watanzania wote wako salama.
Taarifa hii inamaanisha kuwa hatujapata taarifa zozote za Watanzania
walioathirika na janga hili mpaka sasa zaidi ya uharibifu wa mali
kutokana na tetemeko na tsunami. Tumeweza kuthibitisha kuwa watanzania
walioko Fukushima na Sendai (maeneo yaliothirika zaidi) wote wako
salama.
Tutaendelea kutoa taarifa kwa kadri tutakapokuwa tunapata habari mpya.
Kwa wale ambao wangependa kupata taarifa za ndungu zao tafadhali wasiliana nasi kwa kutumia anuani:chairman@tanzanitesociety.jp.
Utakapotuandikia tafadhali tupe
taarifa zifutazo kama unazifahamu: Jina kamili, mji anaoishi na namba
yake ya simu au anunai yake. Unaweza pia kutupa namba yako ili tuweze
kukutaarifu kwa haraka.
Ahsanteni.
Uongozi.
Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani.
|
0 comments:
Post a Comment