Waziri wa Maji,Prof. Mark
Mwandosya (kulia) pamoja na Mkuu wa Jumuia ya Ulaya Nchini Balozi,Tom
Clarke (pili kushoto) wakimsikiliza kwa makini mwandisi mshauri wa
(Consultant) wa maradi wa maji taka katika eneo la Butuja alipokuwa
akitoa maelezo ya mradi huo leo jijini Mwanza.
Na Nurdin Ndimbe,Mwanza
Waziri
Wa Maji Mh. Mark Mwandosya leo amefungua wiki ya Maji mjini hapa kwa
kuzindua mradi mkubwa wa Maji taka katika eneo la Butuja Wilayani
Ilemela Mwanza.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo, Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mwanza
(MWAUASA) Bw. Mashaka Sitta alisema kuwa mradi huo utakaogharimu karibu
Billioni 29 ulibuniwa mwaka 2002 na kuanza kutekelezwa tangu mwaka
2009.Alieleza kuwa miradi itakayojumuisha katika mradi huo ni pamoja na
ujenzi wa bomba kubwa la kipenyo cha mm 700 kwa umbali wa mita
140,ujenzi wa mabwawa mapya matatu, ukarabati wa mabwawa kumi ya zamani,
ujenzi wa matanki mapya ya kuhifadhia Maji taka pamoja na ununuzi wa
vifaa vya maabara.
‘’ Tunatarajia kuwa kukamilika kwa mradi huu
itatuwezesha kujenga pia mtandao wa Maji taka kwa kilomota 24, kujenga
mashimo ya maji taka (manhole chambers) zipatazo 880 itakayounganisha
karibu nyumba 5000 kwenye mtandao wa majitaka’’ alisema Mkurugenzi huyo.
Akizungumza
baada ya uzinduzi huo, Mh Waziri alisisitiza umuhimu wa kutunza miradi
hii kwani Wafadhili wanatumia fedha nyingi kugharamia miradi hii.
‘’Nisingependa baada ya ufunguzi huu wa leo, tuwaombe tena Wafadhili
kutukarabatia miundominu yetu nitashukuru kama kutakuwa na kazi ya mamna
hii katika Nchi moja ya jirani basi kazi hiyo ifanywe na MWAUSA’’
alisisitiza Mwandosya.
Pamoja na uzinduzi huo Mh.Waziri alipokea
pia magari 4 ya kubebea maji taka yatakayotumika na Mamlaka ya Maji Safi
na Maji Taka jiji Mwanza.Sherehe ya UzinduzI wa mradi huu mkubwa maji
taka ulihudhuriwa pia na Mwakilishi mkuu wa Jumiya ya Ulaya hapa
Tanzania Balozi Tom Clarke, Balozi Mdojo wa Ujerumani hapa Nchini pamoja
na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya maendeleo ya Ujerumaini (KWF) Dr
Wolfgang.
Maadhimisho ya wiki ya Maji yanafanyika katika viwanja
vya Nyamagana jijini Mwanza na yatafikia kilele chake tarehe 22 Machi
kwa kufungwa rasmi na Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh. Gharib Bilal.
|
0 comments:
Post a Comment