TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, March 15, 2011

MAHARAMIA WA KISOMALI WAHUKUMIWA MAREKANI…!!!

6:29 PM
Raia watano wa Somalia waliopatikana na hatia ya kutaka kuteka meli ya jeshi la majini ya marekani waliodhania ni meli ya kibiashara wamehukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Watu hao wanaosadikiwa kuwa maharamia wamepatikana na hatia mwezi Novemba kwa kujaribu kuteka meli ijulikanayo kama USS Nicholas, meli iliyokuwa ikifanya doria kudhibiti utekaji wa meli baharini.

Mawakili wa utetezi wamedai kuwa wasomali hao walikuwa wametekwa na maharamia na kulazimishwa kufyatua silaha zao dhidi meli hiyo ya Marekani katika shambulio lililofanyika mwezi Aprili.

Waendesha mashitaka wamesema Wasomali hao wanakuwa wa kwanza kuhukumiwa na mahakama ya Marekani kwa kosa la uharamia tangu mwaka 1820.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA