Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com na ule wa www.shwari.com umepata kutembelea uwanja huo wa Nduli kabla ya ziara mbali mbali za viongozi wa kitaifa na baada ya ziara hizo za viongozi na kushuhudia udanganyifu mkubwa ambao umekuwa ukifanywa na viongozi wa mkoa wa Iringa kwa viongozi hao katika harakati za kuficha aibu ya ubovu wa gari la zima moto katika kiwanja hicho cha Ndege .
Uchunguzi wa kina uliofanywa na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com umebaini kuwa gari linalotumika kwa sasa ambalo ni maalum kwa ajili ya uwanja huo wa Ndege Nduli ni gari aina ya Mazda lenye namba STH 69 34 ni gari la kizamani ambalo limekuwa si msaada wowote katika uwanja huo zaidi ya kusaidiwa na gari kubwa la kikosi cha Zimamoto katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.hapa
0 comments:
Post a Comment