TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, December 20, 2010

NEWS ALERT: mmoja afa na wengine watatu wajeruhiwa katika ajali ya ndege ndogo mbeya

11:40 AM




Picha na habari na
Thobias Mwanakatwa

Ndege hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Tropical-Air Z yenye namba SH-PCN U206F imeanguka majira ya saa 6;39 katika eneo la Uyole nje kidogo na jiji la Mbeya muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege Mbeya kuelekea Dar es Salaam.

Ndege hiyo ilikodiwa na Mfuko wa Bima ya Afya kwa ajili ya kuja kumchukua Mwanafunzi huyo ambaye kwa sasa ni marehemu.

Mwanafunzi huyo aliyefariki amemaliza kidato cha Nne mwaka huu katika shule hiyo ambapo alikuja kuchukuliwa kukimbizwa kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na maradhi.

Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya,Suma Kibopile, alisema kufuatia ajali hiyo wamepokea majeruhi watatu ambao ni pamoja na Dakrati wa Rufaa kitengo cha Mifupa, Dk.Jons Chitemo, ambaye alikuwa akimsindikiza mwanafunzi huyo kumpeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kibopile alisema majeruhi wengine wa ajali hiyo ni Rubani wa ndege hiyo,Keyuln Fakhard raia wa Iran ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kupata mshituko baada ya kupata taarifa kuwa mwanafunzi aliyekuja kumchukua amefariki dunia na Muuguzi Frorence Stephen ambaye ametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mh. Venance Balama, ambaye alifika eneo la tukio amesema kuwa ajali hiyo imeleta historia nyingine kwani mwaka 2006 kulitokea ajali ya ndege katika uwanja huo ambapo Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, Juma Akukweti alipata ajali na kufariki wakati ametoka kuangalia soko la Mwanjelwa lililoungua mwaka huo.

Balama alisema ajali ya ndege iliyotokea jana nayo imekuwa siku chache tu baada ya kuungua kwa Soko kuu la Uhindini mapema mwezi huu.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA