Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Jerry Slaa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikakati na majukumu aliyoyaweka katika kuhakikisha Manispaa ya Ilala inakuwa nzuri na yenye kusifiwa.
Na.MO BLOG TEAM
Meya wa Manispaa ya Ilala katika Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Jerry Slaa amekutana leo na madiwani wa Manispaa hiyo katika kuwashukuru kwa ushindi mkubwa alioupata kwa kumchagua kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo na kupanga mikakati ya utendaji kazi katika Manispaa ya Ilala.
Akizungumza na waandishi wa habari Bw. Jerry Slaa amesema Manispaa ya Ilala ni Manispaa kubwa katika jiji la Dar es Salaa na yenye watu zaidi ya milioni 1 na inakabiliwa na matatizo na kero mbalimbali zinazohitajika kufanyiwa ufumbuzi wa haraka.
Aidha Bw. Jerry Slaa katika kikao chake cha siku ya leo ameunda kamati za kudumu na kamati ndogo ndogo katika kushughulikia kero mbalimbali na kwamba Serikali iipe jicho Manispaa ya Ilala katika kuleta watendaji mahiri watakaoshughulikia mambo mbalimbali ya Mansipaa hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa majengo mbalimbali.
Akihitimisha Bw.Jerry alizungumzia swala la machinga complex na kudai kuwa tatizo si Machinga Complex bali tatizo ni ukosekanaji wa masoko ya kufanyia biashara kwani kama masoko yatakuwepo hakutakuwa na wafanyaji biashara barabarani hivyo kusudi lake ni kuboresha masoko kama vile la Mchikichini na mengineyo katika kutumia utaratibu wa kitaalam kwa kupangisha wafanyabiashara hao.
Afisa Utamaduni Manispaa ya Ilala Bi.Shani Kitogo akiimba shairi mbele ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala linalompa moyo wa kuendelea na kutokuogopa mawimbi kwani ndio mwendo wa ngalawa.
Madiwani wa Manispaa ya Ilala wakimsikiliza Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Anatogulo jijini Dar es Salaam.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Bw. Jerry Slaa akifunga mkutano aliokuwa akizungumza na Madiwani wa Manispaa hiyo juu ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment