TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, November 13, 2010

PSI/Tanzania wazindua sura mpya ya Salama Studs condom

7:48 AM

Mwenyekiti Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dk Fatma Mrisho akijiandaa kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa sura mpya ya kondomu ya Salama Studs, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa PSI/Tanzania, Daniel Crapper.
Na Gaston Shayo
SHIRIKA linalotoa huduma na elimu ya afya nchini chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, PSI/Tanzania limezindua sura mpya ya kondomu yake aina ya Salama Studs, maarufu kama Salama ya Vidutu.

Uzinduzi huo ulifanywa na Mwenyekiti mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS), Dk Fatma Mrisho jijini Dar es Salaam.

Akiongea katika uzinduzi huo, Dk Fatma alisema kuwa kondomu ni moja kinga zinazotegemewa sana katika mapambano dhidi ya kuenea kwa Virusi vya Ukimwi (VVU) hapa nchini na duniani kwa ujumla.

Alisema kuwa ugonjwa wa Ukimwi bado ni tishio na unaendela kuathiri maisha ya maelfu ya wananchi hivyo kutoa wito kwa Watanzania kuchukua hatua za makusudi kujilinda dhidi ya VVU.

Dk Fatma alisema alisema takwimu za kitfaifa zinaonyesha kuwa hali ya maambukizi ya kitaifa ni wastani wa asilimia 5.7, hii ikiwa ni kwa wanaume, na wanawake wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49, kiwango ambacho alisema kuwa ni kikubwa kwa nchi kama Tanzania.

“Tunahitajika kuongeza mapambano na vita hii ngumu, kila mmoja wetu aweke dhamira ya kweli, ndiyo maana leo hii PSI TANZANIA mnapozindua muonekano mpya wa hii kondomu ya Salama, inaonyesha ni jinsi gani mlivyokuwa na dhamira ya kweli katika vita hii ngumu, hongereni,” alisema Dk. Fatma.

Alisema ziko njia nyingi za kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi ikiwemo kuacha ngono na kuwa mwaminifu, njia ambazo zikishindikana basi matumizi sahihi na kila mara ya kondomu ndiyo inakuwa njia pekee ambayo inaweza kunmsaidia mtu kutopata maambukizi ya VVU.

“Kondomu zimekuwa zikitumika hapa nchini kwa muda mrefu sasa, awali zilikuwa zikitumika kama njia ya kupanga uzazi, baada ya kugundulika kwa VVU, tafiti zilifanyika kitaifa na kimatifa na kama ilivyothibitishwa na WHO na UNAIDS ni kwamba kondomu zikitumiwa vizuri zina uwezo mkubwa wa kuzuia maambukizi ya VVU na magonjwa ya zinaa,” alisema Dk. Fatma.

Awali akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi,Mkurugenzi Mtendaji wa PSI TANZANIA, Daniel Crapper alisema walifikia uamuzi wa kubadilisha mwonekano wa kondomuza Salama Stud ikiwa ni kuitikia wito wa watumiaji wake ambao utafiti uliofanywa ulionesha kuwa wengi walitaka kuhakikishiwa juu ya ubora na uimara wa kondomu zinazozambazwa na PSI.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA