TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Sunday, April 4, 2010

Kiongozi wa wazungu Afrika Kusini auwawa

11:13 AM

Kiongozi mwenye msimamo mkali wa wazungu nchini Afrika Kusini, Eugene Terreblanche, ameuwawa katika shamba lake kaskazini magharibi mwa nchi .

Polisi walisema Bw Terreblanche, ambaye alikuwa na umri wa miaka sitini na tisa, alipigwa na kukatwakatwa hadi kufa, katika kile kinacho-onekana kama mzozo juu ya mishahara ambayo haikulipwa.

Watu wawili wameshtakiwa kwa kuumwua kiongozi huyo.

Bw Terreblanche aliongoza chama cha wazungu wenye msimamo mkali cha AWB, ambacho kilishambulia kituo cha World Trade Centre mjini Johannesburg wakati mazungumzo yaliyolenga kumaliza utawala wa wazungu wachache yakiendelea.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, aliyataja mauaji ya kuongozi huyo kama kitendo kibaya, huku akitoa wito kwa raia kujituliza.

Zuma alisema raia wa Afrika Kusini kamwe wasikubali mtu yoyote kuitumia nafasi hii kuchochea uhasama kwa misingi ya rangi.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA