
India leo inazindua sensa ya kuwahesabu raia wake wote, waliozidi umri wa miaka 15.
Wote watapigwa picha na alama za vidole kuchukuliwa, na kisha kuhifadhiwa kwa kutumia mbinu za kisasa za biometric.
Serikali kisha itayatumia maelezo yaliyokusanywa katika kutoa vitambulisho.
Maafisa wa serikali watahitaji kipindi cha mwaka mmoja ili kupata maelezo yote wanayoyataka kuhusiana na jinsia, dini, kazi na elimu, kutoka kwa raia wake bilioni 1.2.
0 comments:
Post a Comment