Kupitia Baraza lao, wanafunzi hao huendesha mijadala katika Nyanja mbalimbali kama vile masuala ya uchumi, mabadiliko ya tabia nchi, malengo ya maendeleo ya millennia, nafasi ya nchi zinazoendelea, ulinzi na usalama n.k. wanafunzi hawa hujenga hoja na kuzitetea hoja hizo katika mijadala hiyo kuligana ‘interest’ ya nchi wanayoiwakilisha.
Kupitia mijadala hiyo, wanafunzi hao hujaribu kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia hivi sasa, kwa kuandaa rasimu za maazimio na kuzijadili rasimu hizo na hatimaye kuzipitisha iwe kwa kuzipigia kura au kwa kuzipitisha kwa kauli moja.
Na ili kufanikisha mijadala ya baraza hilo, wanafunzi hao hufanya utafiti wa nchi zile wanazotaka kuziwakilisha katika baraza hilo pamoja na mada na ajenda mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment