TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, March 29, 2010

Precision Air kuanzisha safari za Afrika Kusini

5:32 PM

Shirika la Ndege la Precision Air, lina mpango wa kununua ndege nyingine aina ya Boeing 737 baadaye mwaka huu na kuanzisha safari za Johannesburg, Afrika Kusini, Lusaka na Harare.

Precision Air pia ina mpango wa kununua ndege nyingine mpya tano aina ya ATR katika kipindi cha miaka miwili ijayo, ikiwa ni sehemu ya mpango wake kabambe wa kuongeza idadi ya ndege zake.

Hayo yalitangazwa mwishoni mwa wiki na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air na Mkurugenzi Mtendaji, Alphonse Kioko, wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa maalum kwa Mawakala wa Precision Air wa usafirishaji ili kuwapongeza kwa mchango wao wa biashara ya shirika hilo.

‘’Tulianza na mpango wa kuboresha ndege zetu mwaka 2006 tulipoingia mkataba wa dola za Marekani milioni 129 na ATR ya Ufaransa ili ituletee ndege mpya saba. Kati ya hizo, tayari tunazo tano na mbili za mwisho zitaletwa mwezi Juni na Julai, mwaka huu," alisema na kuongeza:

‘’Precision Air imekuwa ikipata faida ya zaidi ya asilimia kumi kila mwaka kwa sababu ya mchango wa mawakala wetu wa usafirishaji,’’ alisema.

Kioka alisema watu wanaothubutu kuota ndio watakaohimili ushindani na biashara itatawaliwa na wale wanaothubutu kuota na kutekeleza ndoto zao.

"Ni matumaini yangu tutaendelea kuota pamoja kwa sababu utekelezaji wa ndoto hizo unatoa gawiwo,’’ aliongeza.

Kioko alisema shirika hilo lina mpango wa kuanzisha huduma ya ujumbe wa maandishi kupitia simu za mikononi (SMS) ili wateja wapate taarifa mbalimbali kuhusu safari za ndege kwa urahisi zaidi kupitia simu zao.

Katika hafla hiyo, kampuni ya uwakala wa usafirishaji ya Bon Voyage Travels, ndiyo waliotangazwa washindi wakiongoza kwa mauzo ya tiketi za Precision Air na kupewa tuzo pamoja na mawakala wengine wote kutambua mchango wao kwa biashara ya Precision Air.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA