TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, March 29, 2010

Obama afanya ziara ya gafla Afghanistan

12:14 PM

Rais Barrack Obama wa Marekani amefanya ziara ya gafla nchini Afghanistan na kuonya kuwa jukumu la Marekani nchini humo bado halijakamilika.

Katika mazungumzo na rais Harmid Karzai mjini Kabul, rais Obama, amesema nchi hiyo imepiga hatua kubwa hususan upande wa kijeshi lakini amekiri kuna masuala mengi ambayo yanahitaji kutekelezwa. Rais Obama amesema raia wa nchi hiyo wanapaswa kujitolea zaidi kupambana na ufisadi na kukuza misingi ya utawala wa kisheria.

Baada ya mkutano na rais Karzai, rais Obama aliwahutubia wajeshi wa Marekani katika kambi ya Bagram. Obama aligusia haja ya kukabiliana vikali na wapiganaji wa Taleban pamoja na wale wa Al Qaeda .

Mwandishi wa BBC mjini Kabul amesema tangazo kuwa marekani haitaondoa majeshi yake nchini humo wakati wowote ujao, ni tangazo ambalo lilikuwa likisubiriwa na raia wengi wa nchi hiyo.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA