
Mawaziri William Ruto wa Kilimo na Pro Sam Ongeri wa elimu walisimamishwa kazi na waziri mkuu Raila Odinga kufuatia kashfa ya mamilioni ya dola katika wizara zao.
Hata hivyo rais Mwai Kibaki alibatilisha hatua ya Odinga akisema waziri mkuu hana mamlaka ya kuwasimamisha kazi mawaziri. Ruto na Ongeri wameendelea kujitetea dhidi ya lawama yeyote.
Wakati huo huo Marekani imeonya kuzuka kwa machafuko ya kisiasa nchini Kenya kufuatia mgogoro wa sasa.
Kenya ilikumbwa na machafuko mengine miaka miwili iliyopita kufuatia uchaguzi mkuu uliokumbwa na utata ambapo zaidi ya watu elfu moja walikufa na maelfu kuachwa bila makao.
0 comments:
Post a Comment