Mtu aliyejaribu kumuua Papa John Paul wa Pili yapata miaka 29 iliyopita, anaachiliwa huru kutoka gereza moja nchini Uturuki.Mtu huyo Mehmet Ali Agca, ametumikia kifungo cha miaka 19 nchini Italia kwa kumpiga risasi Papa John Paul na miaka 10 mingine nchini Uturuki kwa shitaka la awali la mauaji.
Sababu ya Bw Agca kutaka kumuua Papa huyo imebakia kitendawili. Kwanza alisingizia idara ya polisi ya Bulgaria kuwa imemtuma na baadaye akaileza mahakama kuwa yeye ni masihi mpya.
0 comments:
Post a Comment