
Bei za hisa katika masoko ya Dubai na Abu Dhabi zimeonesha kushuka kwa kiasi kikubwa katika siku ya kwanza ya biashara tangu Dubai itangaze kwamba inataka kuchelewesha kulipa baadhi ya madeni yake.
Soko la hisa la Dubai lilifunga biashara kwa kiwango cha asilia mia 7 nukta 3. Abu Dhabi nako soko lilifunga kwa asili mia 8 nukta 3, hiki kikiwa kiwango cha chini kabisa kwa soko hilo .
Kushuka kwa bei za hisa a ya kidini za siku nne, wakati kampuni ya uwekezaji inayosimamiwa na serikali Dubai World, kusema inachelewesha kulipa deni lake la karibu dollar bilioni 60.
Benki kuu ya Emarati imesema itazisaidia benki za nchini na zile za kigeni zinaazofanya shughuli zake nchini humo.
0 comments:
Post a Comment