TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, November 9, 2009

Wajerumani wakumbuka ukuta wa Berlin

8:36 PM
Viongozi mbalimbali duniani wataungana na maelfu ya watu kuadhimisha miaka 20 tangu ukuta wa Berlin ulipoangushwa tukio lililomaliza vita baridi.

Sherehe kubwa zitafanyika katika lango la Brandenburg Gate - ikiwa ni alama ya kuunganika upya kwa Ujerumani mwaka 1990.

Ujerumani Mashariki iliyokuwa ikifuata siasa za Kikomunisti, ilijenga ukuta wenye urefu wa kilometa 155 mwaka 1961 kuizunguka na kuitenga na Berlin Magharibi.

Ukuta huo mzito uliwekwa kuwazuia watu kutoka iliyokuwa Ujerumani Mashariki kuukimbia ukomunisti.

Zaidi ya watu 100 inaaminika waliuawa eneo hilo la ukuta walipokuwa wakijaribu kutoroka.

Kikwazo hicho cha ukuta kiliondolewa bila kutazamiwa tarehe 9 mwezi wa Novemba mwaka 1989, baada ya kutokea wiki kadha za maandamano ya kupinga.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA