TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Sunday, November 22, 2009

Mkapa: Majigambo ya uongozi bora kama kuchokoza nyuki

8:01 PM
Na Sadick Mtulya

UAMUZI wa Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kuvunja ukimya na kuzungumzia mazuri aliyoyafanya katika utawala wake, sasa unaonekana kumwigiza katika matatizo zaidi baada ya kutafsiriwa na watu kuwa ni kujisafisha.

Hivi karibuni Mkapa alijisifia kwamba ana sifa za uongozi na kwamba tuhuma zake anamwachia Mungu, baadhi ya wasomi na wanasiasa nchini wameyatafsiri maneno hayo kwamba ni ya kutaka kujinasua katika kashfa zinazomkabili kutaka kuwaachia wananchi wapime nani kafanya mazuri kati yake na Rais Jakaya Kikwete.

Wakizungumza na Mwananchi Jumapili kwa nyakati tofauti jana wadau hao walisema kauli hizo za Mkapa ama zinakwepesha hoja ya msingi ya watanzania kumtaka azungumzie tuhuma zake na zina lengo la kubadalisha ajenda ili waangalie mabaya ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete.

Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Mwesiga Baregu amesema, Mkapa anatakiwa kujitokeza hadharani na kukiri kwa kujibu tuhuma zote zinazomkabili ikiwemo kutolea ufafanuzi maeneo aliyofanikiwa na aliyoshindwa katika utawala wake.Endeleea



0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA