CLUB MAISHA YATEKETEA KWA MOTO!!!
Ukumbi maarufu kwa burudani jijini Dar es salaam, Club Miasha uliyopoa Oysterbay umeteketea kwa moto mchana huu. Habari zilizopatikana muda mfupi uliyopita kutoka eneo la tukio zinsema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa nane adhuhuri na ukumbi mzima wa disco umeteketa kabisa!!! Ukumbi huo umefanyiwa ukarabati mkubwa hivi karibuni na ulikuwa ni ukumbi unaochuana na Club Billicanas kwa viwango na upigaji disco. Picha za tukio zitawajia muda mfupi ujao.
0 comments:
Post a Comment