TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, October 12, 2009

2:49 PM
Watakaopata mikopo ya Elimu ya juu watangazwa
JUMLA ya wanafunzi 18,500 wameidhinishwa kupewa mikopo kati ya idadi ya wanafunzi 24 ,000 wanaokusudiwa kupewa mikopo hiyo kwa ajili ya Mwaka wa masomo 2009/2010 .

Bodi ya mikopo nchini(HELSB )jana ilitoa orodha ya wanafunzi waliofuzu vigezo mbali mbali vilivyokuwa vimetangazwa kwa ajili ya kuomba mikopo hiyo .

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa HESLB , Cosmas Mwaisobwa alisema kuwa mchakato wa kuwapata wanafunzi wengine 5500 waliobakia unaendelea ili kufikisha idadi ya wanafunzi 24,000 watakaopatiwa mkopo huo kwa mwaka huu, ambapo hata hivyo alisema kwamba orodha hiyo iliyobaki inategemewa kutolewa hivi karibuni na bodi hiyo.

Akizungumzia idadi ya wanafunzi waliomba kupatiwa mkopo huo Mwaisoba alisema idadi kubwa ya wanafunzi walijitokeza kuomba mkopo huo kwa ajili ya Mwaka wa masomo wa 2009/2010 na kuongeza kuwa idadi hiyo ilikuwa kubwa kutokana na ukweli kwamba wanafunzi wengi walianza kutuma maombi yao katika kipindi ambacho bado walikuwa shuleni.

Awali akiwasilisha Bungeni makadirio ya Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi ya Mwaka 2009/2010 mapema mwezi ,Waziri Jumanne Maghembe alisema jumla ya wanafunzi 69,442 wa elimu ya juu watapatiwa mkopo wa masomo yao kwa mwaka huu wa fedha ikiwemo idadi hiyo ya wanafunzi 24,000 wanaotarajia kuanza kipindi hiki cha 2009/2010, huku kiwango cha fedha kwa ajili ya kufanikisha mikopo hiyo kikiwa kimeongezwa na serikali na kufikia Sh. 197.3bilioni kutoka Sh. 117 Bilioni, ilizokuwa ikitoa kwa miaka mitatu mfululizo.

Kwa mujibu wa Waziri Maghembe kuhusu mabadiliko ya mwaka huu, wanafunzi wa masomo ya sayansi watakaopata daraja la kwanza hadi la tatu watapatiwa mkopo wa asilimia 100 na wanafunzi watakaochukua kozi ya ualimu watapewa mkopo wote wa daraja la kwanza hadi la tatu lakini kwa utaratibu wa zamani kulingana na uwezo wa kiuchumi ambapo kwa wanafunzi wa masomo mengine watapewa mkopo wa daraja la kwanza na la pili tu.

Alisema katika mwaka huu serikali itakamilisha Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Juu(MMEJU) utakaoanza kutumika katika mwaka wa fedha ujao hadi 2015 na kuongeza "hivi sasa serikali iko kwenye majadiliano na wahisani mbalimbali ili kupata fedha za utekelezaji wa mpango huo’.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA