.jpg)
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Temboni jana jioni walifunga barabara ya Morogoro, wakishinikiza kuwekewa matuta baada ya mwenzao mmoja kugogwa na kufariki dunia.
Kamanda wa mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa 9:00 alasiri eneo la Kimara kwa Msuguri,Jijini Dar es Salaam.
Amesema wanafunzi hao walijikusanya na kwenda hadi njia panda ya Temboni na kisha kuweka magogo barabarani kuzuia magari yasipite.
“Tulipata taarifa na kwenda eneo hilo ambapo tulifanikiwa kuwatawanya na magari yakaanza kupita…hapakuwa na madhara yoyote kwa binadamu,” akasema Kamanda Kalunguyeye.
Akasimulia chanzo cha tukio hilo, Kamanda Kalunguyeye amesema lilisababishwa na mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule hiyo, Sebastian Fabian kugongwa na gari katika barabara hiyo jana saa 5:00 asubuhi.
Akasema mwanafunzi huyo aligongwa na gari aina ya Toyota Land Crusser lenye namba za usajili 371 AZG lililokuwa likiendeshwa na Agustino Mtweve , 40.
“Dereva huyo alimchukua na kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Tumbi kwa matibabu lakini alifariki dunia muda mfupi baadaye,”akasema.
Kamanda amesema mwanafunzi huyo aligongwa wakati akijaribu kuvuka barabara hiyo na gari ambalo lilikuwa likitokea Temboni kuelekea kwa Msuguli.
0 comments:
Post a Comment