TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, October 9, 2009

Rais Obama ashinda tuzo ya Nobel

9:31 PM

Rais wa Marekani, Barack Obama, ndiye mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2009.

Kamati kuu wa tuzo ya Nobel imesema kiongozi huyo ameshinda tuzo hiyo kutokana na juhudi zake kuimarisha uhusiano mwema kati ya watu wa dunia.

Kamati hiyo ilitaja moja wapo wa juhudi za Obama katika kuunga mkono mashirika ya dunia kuafikia kuwepo na ulimwengu bila silaha.

Msemaji wa Bw Obama amesema rais huyo amepokea taarifa hiyo kwa unyeyekevu. Msemaji huyo alimuamsha rais Obama punde tu habari hizo kutangazwa.

Jumla ya watu 205 waliteuliwa kupata tuzo hiyo, akiwemo Waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai na mwanaharakati wa mageuzi nchini Uchina Hu Jia.

Mshindi wa tuzo ya Nobel hupokea medali ya dhahabu, cheti cha diploma na dola milioni 1.4.

Tangu kuchukua hatamu za uongozi rais Obama amesimamia masuala muhimu ya dunia ukiwemo mpango wa amani Mashariki ya Kati na kutoa nafasi ya mazungumzo kuhusu mpango wa Iran wa nukilia.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA