
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayeongoza uchunguzi dhidi ya mauaji ya waandamanaji nchini Guinea amewasili nchini humo.
Afisa huyo, Haile Menkerios anatarajiwa kuendesha uchunguzi kuhusiana na tukio la Septemba 28 ambapo wanajeshi wa Guinea waliwafyatulia risasi waandamanaji.
Makundi ya kutetea haki za binadamu yamesema watu 157 waliuawa mwezi jana.
Hapo jana bw. Menkerios alikutana na kiongozi wa kijeshi, Kapteni Moussa Dadis Camara, waziri mkuu Kabine Komara na wanachama wa upinzani
0 comments:
Post a Comment