TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Sunday, October 4, 2009

Kauli za Salim, Warioba zautikisa utawala wa Kikwete

1:33 PM
AWAZIRI wakuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba na Dk Salim Ahmed Salim walikuwa wakizungumza siku moja wakiwa maeneo tofauti, lakini kauli zao kuhusu uendeshaji nchi wa serikali ya awamu ya nne zilifanana na hakuna shaka kwamba, zimeutikisa utawala wa Rais Jakaya Kikwete.

Wote wawili walitoa kauli zinazoonyesha kuwa nchi inayumba na kwamba vita inayoendelea dhidi ya rushwa haiwezi kufanikiwa kama serikali haitapambana kuuondoa mfumo ambao unalea rushwa, huku wakimuelezea Rais Kikwete kuwa anashauriwa vibaya.

Mara baada ya vyombo vya habari kuchapisha habari ya vigogo hao, mweka hazina wa CCM, Amos Makala alijibu kwa maneno makali, akielekezea shutuma zake kwa Warioba ambaye alimtuhumu kuwa hajawahi kuzungumzia mazuri ya Kikwete na kwamba hata wakati akishikilia nafasi ya waziri mkuu, kulikuwa na matatizo.

Kauli ya Makala ilifuatiwa na kauli ya makamu mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa ambaye alisema Warioba na Dk Salim wanao uhuru wa kutoa maoni yao dhidi ya serikali kama ilivyo kwa wananchi wengine.



0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA