
Aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amesema waliyoongoza ghasia zilizoibuka baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya lazima wafikishwe mahakamani.
Wahusika wakuu wa vurugu hizo watafikishwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita huko Hague, ICC.
Hata hivyo, Bw Annan amesema ni muhimu wengine wahukumiwe Kenya.
Bw Annan alisaidia katika upatanishi wa kuleta amani baada ya ghasia za mwaka 2008 ambapo watu 1,300 waliuawa na 300,000 walihama makazi yao.
Pia ameonya kuwa Kenya inahitaji kuharakiza mabadiliko iwapo wanataka kuepusha ghasia nyingine kuibuka tena.
Katika siku ya mwisho ya ziara yake ya siku tatu nchini Kenya, Bw Annan amesema serikali imemhakikishia kuwa itashirikiana na mahakama ya ICC.
0 comments:
Post a Comment