TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, October 5, 2009

351,958 wa kidato cha nne kuanza mtihani leo

2:28 PM

Jumla ya watahiniwa 351,958 wa kidato cha nne kote nchini, wanatarajia kuanza mtihani wa taifa leo. Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Profesa Jumanne Maghembe, ilisema, kuwa kati wa watahiniwa hao wavulana ni 183,755 sawa na asilimia 52.2 wakati wasichana ni 168,203 sawa na asilimia 47.8.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa idadi ya watahiniwa walioandikishwa kwa mwaka huu imeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana.

Imesema idadi hiyo imeongezeka kwa 110,486 sawa na ongezeko la asilimia 45.76 ikilinganishwa na mwaka jana ambapo jumla yao ilikuwa ni 241,472.

"Jumla ya watahiniwa wa shule waliojiandikisha kufanya mtihani leo ni 254,355 wakiwemo wasichana 116,806 sawa na asilimia 45.92 na wavulana 137,549 sawa na asilimia 54.08 wakati mwaka jana watahiniwa wa shule walikuwa 166,443, hivyo ongezeko la watahiniwa wa shule ni 87,912 sawa na ongezeko la asilimia 52.82," imebainisha taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea walioandikishwa mwaka huu kufanya mtihani huo ni 97,603 ikilinganishwa na watahiniwa 75,027 walioandikishwa mwaka jana.

Aidha ongezeko la watahiniwa wa kujitegemea ni 22,574 sawa na asilimia 30.09.

"Mtihani wa Maarifa unatarajia kufanyika nchini kote Alhamisi ya wiki hii ambapo jumla ya watahiniwa 24,979 wamejiandikisha kuufanya mtihani huo ambapo wasichana ni 14,702 sawa na asilimia 58.86 wakati wavulana ni 10,277 sawa na asilimia 41.12, hivyo, ongezeko la watahiniwa wa somo hilo ni 1,713 sawa na asilimia 7.36," ilifafanua taarifa hiyo.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA