TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, September 25, 2009

6:47 PM

Mamilioni yamwagwa kwa wanaoishi na VVU K`ndoni


Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetumia zaidi ya Sh. Milioni 25 kuhudumia watu wanaoishi na virusi vya ukimwi katika kipindi cha miezi mitatu pekee.

Aidha, halmashauri hiyo imesema kiasi hicho cha fedha kimetumika katika maeneo muhimu 15, ikiwa ni pamoja na kufanya utambuzi wa watoto yatima na kuwasaidia vifaa vya shule yatima wapatao 1,350 pamoja na vikundi vya wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Bw. Joel Mahyenga, amesema kupitia katika kamati yake ya kudhibiti ukimwi, kiasi hicho cha fedha kimetumika kati ya Aprili na Juni mwaka huu.

Amesema fedha hizo ni kati ya zaidi ya Sh. Mil.139.7 zilizotolewa na hazina ili kufanikisha mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi katika manispaa yao.

"Pia fedha hizo zimewezesha kuvijengea uwezo vikundi vya wanaoishi na virusi vya ukimwi na kuwezesha kufanyika kwa vikao vya robo mwaka vya kamati za ukimwi ngazi ya kata," akasema.

Aidha, maeneo mengine yaliyofanikishwa na kamati hiyo ni ununuzi wa vifaa vya ofisi za mratibu wa kamati ya ukimwi ngazi ya manispaa, mafunzo ya siku tano kwa waelimishaji rika, warsha kwa wafanyakazi kuwajengea ufahamu dhidi ya ukimwi na mafunzo rejea kwa watoa huduma kuhusu kupunguza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua.

Ikifafanua zaidi, taarifa hiyo imesema jumla ya watoa huduma 80 wamenufaika na mafunzo kuhusu ukimwi huku vifaa kadhaa vya ofisi vikinunuliwa.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA